Sistiinho: Outtara ni Mbadala Sahihi wa Serge Wawa, Yanga Hawana Tatizo Lolote

MCHAMBUZI wa soka kupitia kipindi cha Krosi Dongo na Sports Zone kinachorushwa na studio za 255Global Radio na Global TV Sistiinho, amesema mlinzi mpya aliyesajiliwa na kikosi cha Simba kutoka klabu ya Al Hilal ya Sudan Mohamed Outtara ni mbadala sahihi wa beki wa zamani wa klabu hiyo Serge Pascal Wawa.
“Outtara ni beki mwenye profile kubwa ameshacheza mashindano makubwa na Simba kwa hizi siku za karibuni wamemrelease Pascal Wawa moja kati ya mabeki bora kwa kipindi cha miaka minne ya mafanikio ya Simba hiyo inakupa picha ni mchezaji wa aina gani ambaye Simba walimmisi kwahiyo replacement yake sahihi wameona wamtafute beki mwingine wa kimataifa ambaye ni Outtara.” Amesema Sistiinho.

Mohamed Outtara ni beki wa zamani wa miamba ya soka barani Afrika klabu ya Wydad Casablanca ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ambaye kwa mujibu wa historia ni kwamba ameshawahi kufanya kazi pamoja na kocha wa sasa wa Simba SC Zoran Maki wote wakiwa pamoja katika klabu ya Wydad Casablanca.

Kwa upande mwingine Sistiinho ameonesha kuwa na imani na maandalizi ya klabu ya Yanga yakujiandaa na msimu mpya ingawa kumekuwa na maneno kuwa Yanga SC wamechelewa kuingia kambini wanaweza kufanya vibaya tofauti na timu nyingine kama wapinzani wao wakubwa klabu ya Simba ambao wapo nchini Misri tangu Julai 15.

