The House of Favourite Newspapers

“Sweety” Ya Nandy na Jux Yazua Gumzo Mitandaoni – Video

0

Staa wa muziki wa Bongofleva Nandy kwa kushirikiana na Juma Jux wameachia rasmi video ya wimbo wao mpya “Sweety”, ambao kwa sasa unazua gumzo kubwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari vya burudani.

Video hiyo iliyotoka kupitia YouTube imejaa mvuto wa kimapenzi na ubunifu wa hali ya juu, ikiwasogeza mashabiki karibu zaidi na hadithi ya wawili hao wanaoonekana kutengeneza chemistry ya kipekee kila wanaposhirikiana.

“Sweety” ni mchanganyiko wa sauti tamu za RnB na ladha ya Bongo Fleva, huku mashairi yake yakibeba ujumbe wa mapenzi ya dhati na mshikamo wa wapenzi. Wimbo huu umekuja wakati ambapo mashabiki bado wanakumbuka ushirikiano wao wa nyuma uliotikisa vichwa vya habari na kuibua maswali kuhusu uhusiano wao nje ya muziki.

Kwenye mitandao ya kijamii, mashabiki wamekuwa wakimwaga maoni ya pongezi huku wengine wakikiri kwamba Jux na Nandy ni moja ya perfect duo kwenye burudani ya Bongo, na kwamba “wanapokutana, lazima kutoa kitu kikubwa.”

Leave A Reply