Taifa Stars Waweka Historia, Wapokelewa na Viongozi wa Serikali Dar (Picha +Video)

Viongozi mbalimbali wa Serikali, wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi, walipokea kwa shangwe Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, pale walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Januari 8, 2025.
Timu ya Taifa ya Tanzania imeandika historia kwa kufuzu kwa mara ya kwanza hatua ya 16 bora katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), ikiwapa mashabiki wake na taifa kwa ujumla sababu ya kujivunia. Tukio hili limeashiria hatua kubwa kwa soka la Tanzania na kuonesha maendeleo makubwa ya mchezo huo nchini.
Waziri Prof. Kabudi alimpongeza kikosi chote kwa jitihada zao, akisisitiza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya kuunga mkono vijana na kuendeleza vipaji vya michezo nchini.



