The House of Favourite Newspapers
gunners X

Tarimba Aanika Kilichoibeba SportPesa TZ

0
Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (kulia),  akimkaribisha Mkurugenzi wa Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba, katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

ABBAS TARIMBA, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, amesema mafanikio makubwa ya kampuni hiyo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ushirikiano wanaoupata kutoka kwa wadau wake wa karibu ikiwa ni pamoja na Kampuni ya Global Publishers.

Saleh Ally akimpa maelekezo Tarimba baada ya kumpokea. Kulia kwake ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya, na kushoto ni Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.

Ameyasema hayo leo alipotembelea Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori Dar es Salaam ambapo ziara hiyo imekuja katika kutimiza miaka mitatu kwa Kampuni ya SportPesa Tanzania.

Kiongozi Msaidizi wa Global TV online, Amos Chrispine,  akimpa maelekezo Tarimba kuhusu jinsi  namma ambavyo vijana hao wa Televisheni namba moja ya Mtandaoni Tanzania wanavyochakata habari na kuzirusha.

“Tumekuwa tukifanya kazi kwa ukaribu na watu mbalimbali, na tulianza taratibu kwani kulikuwa kuna kampuni nyingine ambazo zinafanya kazi, ila kwa ushirikiano mkubwa ambao tumekuwa tukiupata kutoka kwa wadau  na Kampuni ya Global hasa kwa upande wa magazeti ya michezo ambayo ni Championi na SpotiXtra, tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kutoka kushoto ni Sabrina Msuya, Mtangazaji wa +255 Global Radio na Global TV Online, Kissa Daniel, Abbas Tarimba na mrusha matangazo wa Global TV Online na +255 Global Radio, Hope Ezekiel.

 

“Mbali na kufanya kazi kwa mafanikio makubwa pia tumekuwa tukilipa kodi kwa Serikali zaidi ya bilioni, hivyo sio kitu kidogo hasa ukizingatia kwamba maendeleo ya Serikali yanahitaji kodi nasi pia tumekuwa tukilipa kodi.

Tarimba na Sabrina wakiwa nje ya Studio za +255 Global Radio.

 

“Wadau ambao wapo pamoja nasi tunaomba ushirikiano wao kwani bado tunazidi kupambana ili kuwa bora na mambo yote tunayafanya kwa weledi na kuzingatia kanuni ambazo zipo,” amesema Tarimba.

Saleh na Tarimba wakiwa ndani ya Studio za +255 Global Radio.

 

Mbali na kusema hayo, Tarimba aliongeza kuwa amekuwa akiyafuatilia magazeti ya michezo yanayochapishwa na Global Group ambayo ni Championi na SpotiXtra, huku akiwasihi waandishi wazidishe juhudi zaidi.

Mrisho na Tarimba wakiwa ndani ya Studio za +255 Global Radio.

“Nimekuwa nikiyafuatilia magazeti ya michezo ya Championi na SpotiXtra, mbali na kwamba ni washirika wetu ambao tunafanya nao kazi kwa ukaribu bado magazeti haya yamekuwa na muonekano bora, ubora wa kazi pamoja na yale yanayoandikwa hivyo, cha msingi ni kushikilia hapo ili kuzidi kuwa bora zaidi.”

Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula akisalimiana na Tarimba  na Sabrina.

 

Mhariri wa Gazeti la Ijumaa na Ijumaa Wikienda, Sifael Paul, akisalimiana na Tarimba.

PICHA NA MUSA MATEJA | Global Publishers

Leave A Reply