Tekno Kuungana na Ali Kiba, Wiz Kid, Davido na YCEE
NIGERIA: Taarifa ambazo zipo chini ya carpet ni kwamba msanii wa muziki nchini Nigeria, Tekno ataungana na wasanii wengine wakali kama Davido, Wizkid na Alikiba kwenye Lebo ya ‘Sony Music’.
Mkali huyo wa ngoma ya ‘Pana’ inawezekana akajiunga ‘Sony Music Global’ hivi karibuni.
Kwa mujibu wa post aliyoweka boss wa Upfront & Personal, muanzilishi wa tamasha la ‘One Afrika’ Paul O akiwa kwenye makao makuu ya label hiyo kubwa duniani, New York amedai Tekno anasaini dili kubwa na Sony Music Global.
Iwapo Tekno atafanikiwa kusaini na Sony basi atakuwa ameungana na Davido, Wizkid, Alikiba na Ycee aliyesaini wiki chache zilizopita.


Comments are closed.