TFF Yaruhusu Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Kutumika Kwa Michezo ya Ligi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeruhusu uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, uliopo mkoani Tabora, kutumika kwa michezo ya Ligi baada ya kufanyiwa marekebisho yaliyokidhi viwango vya kikanuni na kisheria vya mpira wa miguu.
Awali, uwanja huo ulikuwa umefungwa kutokana na miundombinu yake kutokidhi vigezo vilivyowekwa katika masharti ya Kanuni na Leseni za Klabu baada ya marekebisho yaliyofanyika kwa kuzingatia maelekezo ya TFF, sasa umethibitishwa kuwa unakidhi viwango vinavyohitajika kwa michezo ya Ligi.
TFF inaendelea kuzikumbusha klabu zote kuboresha na kutunza miundombinu ya viwanja vyao vya nyumbani, ikiwemo kushirikiana na wamiliki (hasa kwa klabu ambazo hazimiliki viwanja), ili kuhakikisha michezo ya Ligi inachezwa katika viwanja bora vitakavyoongeza ushindani na thamani ya Ligi.