The House of Favourite Newspapers

TFF Yatangaza Orodha ya Awali ya Wagombea Uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu (TPLB)

0

Dar es Salaam, Oktoba 10, 2025 — Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kupitia Kamati yake ya Uchaguzi, limetangaza orodha ya awali ya wagombea waliorejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Benjamin Kalume, mchakato wa usaili wa wagombea hao utafanyika Oktoba 15, 2025, jijini Dar es Salaam.

Wagombea hao wanatoka katika makundi tofauti, wakiwania nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, pamoja na wawakilishi wa klabu wanachama wa TPLB.

Kwa upande wa nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi, majina matatu yametajwa:

  1. Nassor Idrissa Muhamed

  2. Said Suud Said

  3. Hoseah Hopaje Lugano

Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, wagombea waliopitishwa katika orodha ya awali ni wawili:

  1. Kheri Nassor Missinga

  2. Hassan Ramadhan Muhsin

Kwa mujibu wa Kamati ya Uchaguzi, baada ya hatua ya usaili kukamilika, orodha ya mwisho ya wagombea watakaothibitishwa kuwania nafasi hizo itatangazwa rasmi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa TPLB.

Leave A Reply