The House of Favourite Newspapers
gunners X

Trump Aogopa Mashtaka ya Kikatiba, Aelekeza Macho Uchaguzi wa 2026 – Video

0
Rais wa Marekani, Donald Trump

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametoa onyo kali kwa wabunge wa chama chake cha Republican, akidai kuwa wasiposhinda uchaguzi wa katikati ya muhula wa Novemba 2026, wapinzani wake wa chama cha Democratic watamng’oa madarakani kwa kumfungulia mashtaka ya kikatiba.

Akizungumza Jumanne katika mkutano wa ndani wa wabunge hao mjini Washington, Trump alisisitiza umuhimu wa ushindi huo ili kulinda ajenda zake na kuepuka uchunguzi wa bunge.

“Lazima mshinde uchaguzi wa katikati ya muhula, kwa sababu msiposhinda, watatafuta sababu yoyote ya kuniondoa madarakani. Nitang’olewa,” Trump amewaambia wabunge hao kwa uwazi.

Katika hotuba yake iliyodumu kwa dakika 84, Trump amewataka washirika wake kuweka kando tofauti zao na kujikita katika kuuza sera za chama kuhusu masuala ya jinsia, huduma za afya, na uadilifu wa uchaguzi, hasa kwa wapiga kura wenye hasira juu ya kupanda kwa gharama za maisha. Amekiri kuwa kihistoria, rais aliyeko madarakani huwa anapoteza viti vingi katika uchaguzi huo, akishangazwa na mwelekeo huo wa fikra za umma.

Huku akijivunia operesheni ya kijeshi dhidi ya kiongozi wa Venezuela, Nicolas Maduro, Trump amekuwa akishinikizwa kuelekeza nguvu zake kwenye masuala ya ndani kama mfumuko wa bei. Hata hivyo, amedai kuwa alirithi tatizo hilo kutoka kwa Democrats na kuwataka Republicans kujivunia kupaa kwa masoko ya hisa.

Trump, ambaye amewahi kufunguliwa mashtaka ya kikatiba mara mbili katika muhula wake wa kwanza (2017-2021) na kuachiwa huru na Baraza la Seneti, kwa sasa anakabiliwa na tishio jipya huku baadhi ya wabunge wa Democratic wakishaanza kuandaa hati za mashtaka dhidi yake kwa madai ya matumizi mabaya ya madaraka katika muhula wake wa pili.

MAPYA! MKUBWA FELLA ANAHITAJIKA KWENDA TENA INDIA – MKE WAKE AWALILIA WATANZANIA na RAIS SAMIA…

Leave A Reply