Uchunguzi wa Mauaji ya Msichana wa Miaka Tisa Aliyechomwa Kisu Lincolnshire, Uingereza Wafunguliwa Rasmi

UCHUNGUZI wa Mauaji umeanzishwa baada ya msichana wa Miaka Tisa kufariki kutokana na jeraha la kudungwa na kisu huko Boston Siku ya Alhamis saa 12:20 Jioni.
Maafisa waliitwa katika eneo la tukio, kwenye eneo la Fountain Lane mwendo wa saa 12:20 siku ya Alhamisi.
Maafisa hao walionekana wakifanya kazi katika eneo la tukio Siku ya Alhamisi jioni, Kabla ya kuondoka alfajiri ya ijumaa, pia kulikuwa kuna kitu kikubwa kilichofunikwa katikati ya Uchochoro kilichokuwa na alama ndogo za njano kikilindwa na Maafisa wa Polisi.

Kifo hicho kilitokea katika sehemu ya Kibiashara ya Boston yenye Nyumba chache sana za Makazi ya Watu, alisema mwandishi wa Sky Frazer Maude.
Pia Polisi wa Lincolnshire walinukuliwa wakisema:

“Tumeanzisha uchunguzi wa Mauaji eneo hilo limezingirwa na tutakuwa kwenye eneo la tukio kwa siku zijazo”
Biashara nyingi katika eneo la tukio ambapo Mauaji hayo yametokea nchini humo zimefungwa kabisa wakati Maafisa hao wa Jeshi la Polisi wakiwa wanaendelea na uchunguzi juu ya mauaji ya msichana huyo, pia Kamba zenye rangi ya njano zimefungwa kuzunguka eneo hilo uku Maafisa wa Polisi wakiwa wametapakaa katika eneo hilo.

