Uteuzi: Rais Samia Ateua Majaji Wa Mahakama Za Rufani, Mahakama Kuu

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama za Rufani Nchini. Walioteuliwa ni, Jaji Lameck Michael Mlacha ambaye alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kigoma na Jaji Paul Joel Ngwembe aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Morogoro
Pia, Rais amewateua Jaji Mustafa Kambona Ismail aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu, Dares Salaam na Jaji Abdul-Hakim Ameir Issa aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Zanzibar
Pia Rais amefanya uteuzi wa Majaji Wa Mahakama Kuu, Walioteuliwa ni aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa, aliyekuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Rufani-DSM, Wilbert Martin Chuma na aliyekuwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania-DSM, Sharmillah Said Sarwat
Pia, Arnold John Kirekiano, aliyekuwa Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania-DSM, Martha Boniface Mpaze, aliyekuwa Naibu Msajili wa Mahakama Jumuishi katika Masuala ya Mirathi na Familia-DSM na Ferdinand Hilali Kiwonde, aliyekuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu
Vilevile, Said Rashid Ding’ ohi aliyekuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania-Iringa, Dkt. Angelo Kataraiya Rumisha, aliyekuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania-DSM, Sarah Duncan Mwaipopo aliyekuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali-DSM na Ntuli Lutengano Mwakahesya aliyekuwa Naibu Karani wa Baraza la Mawaziri, Ofisi ya Rais Ikulu-Dodoma.