Video: Wachina Waliokamatwa Na Maburungutu Ya Pesa, Takukuru Wabaini Ni Za Utapeli

Kamanda wa TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni, Christian Nyakizee, ametoa ufafanuzi kuhusiana na sakata la mabilioni ya fedha linalowahusisha raia wawili wa China wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha katika Mahakama ya Kisutu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Christian Nyakizee amesema Wachina hao wamekuwa wakitafutwa kwa muda mrefu, na kwamba fedha walizokamatwanazo zinashukiwa kuwa ni mazalia ya fedha zilizotakatishwa kupitia fedha za Kadi za Benki zilizoibiwa kutoka kwa watu mbalimbali
Katika hatua nyingine, Nyakizee amesema taarifa iliyotolewa awali na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Oysterbay haikuwa sahihi, kwakuwa yeye aliitwa tu kwaajili ya kushuhudia hivyo taarifa aliyokuwa ameisambaza mitandao awali ipuuzwe na ichukuliwe taarifa rasmi iliyotolewa na mamlaka,
Ikumbukwe kuwa, tayari jioni ya leo Wachina hao wamefikishwa Mahakamani na kusomewa makosa mawili ya uhaini, na sasa wamepelekwa gerezani kwakuwa mashtaka yanayowakabili hayana dhamana.

