Vodacom Yatoa Pole Kwa Familia Ya Athuman Hamis
Kampuni ya Vodacom Tanzania inatuma salamu za pole kwa familia ya aliyekuwa mpigapicha wa magazeti ya serikali ya Daily News na Habari Leo, Athumani Hamis Msengi, aliyefariki jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Vodacom Tanzania PLC pamoja na taasisi yake ya kuhudumia jamii ya Vodacom Tanzania Foundation imepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha Athumani Hamis na inatoa pole kwa familia, mwajiri na wadau wote wa tasnia ya habari.
“Kifo chake cha ghafla kimetuhuzunisha sana ikizingatiwa kuwa marehemu alikuwa akishirikiana nasi wakati wote kwa karibu katika kipindi chote ambacho alikuwa bado hajapata ajali na baada ya kupata ajali tumekuwa naye karibu”
Daima tutaendelea kumkumbuka marehemu Athuman Hamis na tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi na tupo pamoja na familia katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Imetolewa na kitengo cha Uhusiano
Vodacom Tanzania PLC
Comments are closed.