The House of Favourite Newspapers

Wabunge Wataka Wazee wa Mabaraza Kuongezewa Posho

0

WABUNGE wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wameishauri Serikali kurejea upya viwango vya posho za wazee wa mabaraza ya Sh5,000 kwa kesi wakidai ni fedha kidogo.

 

Hayo yameyasema  leo Jumatano Aprili 28, 2021 na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti, Sillo Baran wakati akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya mfuko wa mahakama kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

 

Amesema kamati inaendelea kuishauri Serikali kuhusu kurejewa upya kwa viwango vya posho za wazee wa mabaraza ambao wanalipwa Sh5,000 tu kwa kesi kiasi ambacho ni kidogo ikizingatiwa muda unaochukua kesi kuamuliwa.

 

“Hatua hii itasaidia kuziba mianya ya rushwa lakini pia itaongeza motisha, tija na ufanisi katika kazi za mabaraza husika,” amesema.

Leave A Reply