NEW UPDATES: Watu 179 kati ya 181 Wafariki katika ajali ya ndege Korea Kusini – (Picha + Video)

WATU 179 kati ya 181 hadi sasa wamethibitika kufariki dunia baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupata ajali wakati inatua katika uwanja wa ndege wa Muan nchini Korea Kusini ilipokuwa ikitokea Bangkok, Thailand.
Ajali hiyo ilitokea Jumapili saa 3:03 asubuhi kwa saa za eneo hilo (sawa na 00:03 GMT) wakati Ndege ya Jeju Air, iliyokuwa imebeba abiria 175 na Wafanyakazi sita kutoka Bangkok, mji Mkuu wa Thailand, ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muan, takriban kilomita 289 (maili 179) Kusini Magharibi mwa mji mkuu wa Seoul.
Abilia wawili tu walikuwa wa Thailand na wengine wote walikuwa wa Korea Kusini.
Wafanyakazi wawili, mwanamke na mwanaume walipatikana wakiwa hai ni wafanyakazi wa ndege hiyo na wamekimbizwa hospitali iliyo karibu na uwanja huo.



