Watu 220 Wauawa Kwenye Mapigano ya Kikabila Nchini Sudan Kusini

WATU 220 wameuawa kwenye mapigano ya kikabila yaliyotokea nchini Sudani Kusini na kutajwa kuwa hayo ni miongoni mwa mapigano mabaya zaidi ya kikabila kuwahi kutokea hivi karibuni nchini humo.
Taarifa hiyo imetolewa na Afisa wa Afya ya nchi hiyo na kueleza kuwa mapigano hayo yalitokea katika Mkoa wa Blue Nile, unaopakana kati ya Ethiopia na Sudan Kusini.
Mapigano hayo yaliyosababishwa na mgogoro wa ardhi yalitokea mapema mwezi huu ambapo yalihusisha kabila la Hausa lenye mizizi yake Afrika Magharibi, dhidi ya watu wa kabila la Berta.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Fath Arrahman Bakheit, mzozo huo ulipamba moto Oktoba 19 na 20, mwaka huu katika Mji wa Wad el-Mahi, uliopo kwenye mpaka na Ethiopa.
Bakheit ameliambia Shirika la Habari la Associated Press kuwa hadi kufikia siku ya Jumamosi maafisa walihesabu maiti takribani 220 na kueleza kuwa idadi ya watu waliofariki dunia huwenda ikaongezeka kwa sababu timu za madaktari hazikufika kwenye eneo la mapigano.
Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

