Waziri Mkuu Apokea Shilingi Milioni 20 Kusaidia Waathirika Mkoani Kagera
Waziri Mkuu wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni ishirini kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya CHIGO, Guo Zhijian (kulia). Kwa habari kamili tembelea Global TV Online.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi hao.
Majaliwa akizungumza na wanahabari mara baada ya kupokea hundi
ya shilingi milioni ishirini kutoka kwa kampuni ya ujenzi wa barabara ya Kichina.
Majaliwa akimpatia mkono wa shukrani kwa msaada huo mwakilishi wa kampuni hiyo ya kichina, Guo Zhijian.
Wakiendelea kupiga picha za pamoja.
Mmoja wa wanajumuiya ya wahindi wanaofanya shughuli za viwanda hapa nchini,
Gagan Gupta (kushoto) akimpa mkono Waziri Majaliwa.
Kassim Majaliwa leo amepokea msaada wa shilingi milioni ishirini kutoka kwa kampuni moja ya kichina inayoshughulika na ujenzi iitwayo China Henan International Cooperation Group Ltd (CHIGO).
Kampuni hiyo imekabidhi mchango wake kwenye ukumbi uliopo katika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, mwaka huu mkoani Kagera.
Pia katika makabidhiano ya msaada huo, walikuwepo wanajumuiya ya wahindi wanaofanya shughuli za viwanda hapa nchini (Camal Steels Ltd) ambao waliahindi kuingiza kiasi cha shilingi milioni ishirini katika akaunti maalum ya maafa ya mkoani Kagera.
Akizungumza na wanahabari baada ya kupokea hundi ya msaada huo, Majaliwa alisema anaishukuru kampuni hiyo ya CHIGO na jumuiya hiyo ya wahindi kwa ahadi yao ya shilingi milioni ishirini kwani zitawezesha kwa namna moja ama nyingine kupunguza makali ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera na kusisitiza kuwa misaada bado inaendelea kupokelewa.
Na Denis Mtima/Gpl




Comments are closed.