The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Atoa Siku Tano kwa Wizara ya Kilimo Kuondoa Pikipiki Wizarani

0
Waziri Mkuu, akikagua pikipiki zilizopo katika Ofisi za Wizara ya Kilimo jijini Dodoma, Juni 8, 2022, ambazo zilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Maafisa Ugani kote nchini. Waziri Mkuu ameiagiza Wizara hiyo ihakikishe ifikapo Juni 12, 2022 (Jumapili) ziwe zimeshakabidhiwa kwa Maafisa Ugani. Kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Profesa Siza Tumbo.

 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ametoa siku tano kuanzia leo Juni 8, 2022 hadi Juni 12, 2022 kwa Wizara ya Kilimo iwe imeondoa pikipiki zote wizarani hapo na kuzikabidhi kwa wakurugenzi. Pikipiki hizo zimetolewa kwa ajili ya maafisa ughani kote nchini.

 

Ametoa agizo hilo leo Juni 8, 2022, alipokagua Ofisi za Wizara ya Kilimo zilizopo eneo la VETA, Dodoma na kukuta pikipiki zilizotolewa kwa ajili ya maafisa ughani zikiendelea kuwepo.

“Hii haikubaliki, Wakurugenzi wote waandikiwe barua waje wazichukue, kama kuna ufungaji wa plate number utafanyika huko huko, Jumapili saa 10:00 jioni ziwe zimefika kwa wahusuka,”ameagiza Waziri Mkuu.

 

Amesema tayari Rais Samia alishazikabidhi kwa ajili ya kupelekwa kwa maafisa ugani, hivyo kitendo cha pikipiki hizo kuendelea kubaki katika eneo hilo hakikubaliki.

 

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Profesa Siza Tumbo, amemhakikishia Waziri Mkuu kwamba wamepokea maelezo hayo na watayafanyia kazi.

MAUJI YA WANAWAKE: WANAHARAKATI, MAKUNGWI WAFUNGUKA SABABU ZINAZOPELEKEA MAUAJI | MAPITO

Leave A Reply