Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Aongoza Mkutano Kazi wa Mawaziri na Makatibu Wakuu Dodoma

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameongoza mkutano kazi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu na Viongozi Waandamizi wa Serikali uliofanyika, Januari 12, 2026, katika Ukumbi wa Kambarage, Hazina, jijini Dodoma.
Katika mkutano huo, viongozi hao wamejadili utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Serikali yanayolenga kuimarisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.


