The House of Favourite Newspapers
gunners X

Waziri wa Afya wa Ureno Ajiuzulu Baada ya Mtalii Mjamzito Kufariki kwa Kushindwa Kuhudumiwa

0
Waziri wa afya wa Ureno Dkt.Marta Temido amejiuzulu

Waziri wa afya wa Ureno, Dkt.Marta Temido amejiuzulu saa chache baada ya ripoti kuibuka kuwa mtalii mjamzito amefariki dunia. Mwanamke huyo wa India mwenye umri wa miaka 34 aliripotiwa kufariki dunia baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo alipokuwa akihamishwa kutoka Hospitali ya Santa Maria ya Lisbon ambayo ni hospitali kubwa zaidi nchini Ureno kwa sababu kitengo chake cha watoto wachanga kilikuwa kimejaa.

Alikuwa akihamishwa kutoka Hospitali ya Santa Maria ya Lisbon

Dkt.Marta Temido alikuwa waziri wa afya wa Ureno tangu 2018, na anasifiwa kwa kuiongoza Ureno kupita janga la Uviko-19, lakini baada ya mfuatano wa matukio yanayo chafua wizara ya afya siku za hivi karibuni, serikali ilitoa taarifa kwamba Dkt Temido “ametambua kwamba hakuwa na ulazima tena wa kusalia ofisini”.

 

Kumekuwa na visa kama hivyo nchini Ureno katika miezi ya hivi karibuni ikiwa ni pamoja na vifo tofauti vya watoto wachanga wawili ambao mama zao walikuwa wamehamishwa kati ya hospitali na kushindwa kuvumilia kucheleweshwa kwa muda mrefu.

Kumekuwa na mfuatano wa matukio yanayoichafua wizara ya afya

Serikali imetoa taarifa ya upungufu wa watumishi wa afya nchini Ureno hususani waliobobea katika masuala ya magonjwa ya wanawake na uzazi ambapo inafikiria kuajiri kutoka nje ya nchi.

 

Imeandikwa na:John Mbwambo kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply