Yanga Wafanya Mazoezi Kwenye Fukwe za Coco Beach
CLATOUS Chama ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga akitokea Simba tayari yupo kambini na wachezaji wengine kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2024/25 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ni jezi namba 20 alionekana kuanza nayo kazi kwenye mazoezi yaliyofanyika fukwe za Coco Beach Julai 10 2024 ambapo huko alikutana na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Jezi hiyo kwa msimu wa 2023/24 alikuwa anavaa mwamba wa kazi ngumu kwenye eneo la kiungo anaitwa Zawad Mauya.