The House of Favourite Newspapers
gunners X

Yanga Yawa Klabu ya Kwanza Kujiunga na Jumuiya Mpya ya Vilabu Afrika (ACA)

0

Klabu ya Yanga SC imeingia kwenye historia baada ya kuwa mwanachama wa kwanza kujiunga rasmi na Jumuiya ya Vilabu vya Afrika (African Clubs Association – ACA), taasisi mpya iliyozinduliwa kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano na maendeleo ya soka la vilabu barani Afrika.

Mabingwa hao wa Tanzania wamekamilisha ada ya uanachama ya Shilingi milioni 2.4 (sawa na Dola 1,000), hatua inayowaweka katika nafasi ya kuwa miongoni mwa vilabu vinavyoanzisha na kusimamia mwelekeo mpya wa maendeleo ya soka la ushindani barani.

Kwa mujibu wa ACA, lengo la jumuiya hiyo ni kuunganisha vilabu vya Ligi Kuu na Daraja la Kwanza katika mataifa mbalimbali ya Afrika ili kubadilishana mbinu, kuimarisha mifumo ya usimamizi, kuongeza ushindani na kuipa vilabu sauti kwenye masuala ya maendeleo ya soka la bara hilo.

ACA imezitaka klabu zote barani Afrika, hususan zinazoshiriki ligi za juu, kuungana katika mpango huo ili kujenga nguvu ya pamoja itakayoboresha zaidi mashindano, masoko na ustawi wa vilabu.

MWANA-FA MSIBANI kwa MAMA wa CRAZY GK – AFICHUA WALIVYOTUPIWA CHUPA STEJINI….

Leave A Reply