The House of Favourite Newspapers
gunners X

Zaidi ya Watu 12 Wameuawa Congo Katika Mashambulizi Tofautitofauti

0
Waasi nchini Congo wamekuwa wakiwalenga raia na kuwaua

ZAIDI ya watu 12 wameuawa huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo katika mashambulizi yaliyotokea mashariki mwa nchi hiyo siku 3 zilizopita.

 

Kiongozi mmojawapo wa jeshi katika jimbo la Kivu kaskazini ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa kuna mwanajeshi mmoja aliuawa katika shambulio kaskazini mwa mji wa Butembo na wanamgambo wa mai-mai , pia aliongezea kuwa wapiganaji wengine wawili wa kundi hilo waliuawa katika  shambulio hilo.

Makundi ya waasi nchini Congo yanatekeleza mauaji ya raia katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo

Jana Rais wa mashirika ya kiraia huko Lodjo katika jimbo la Huri prince Kaleta wakati akizungumza na shirika la habari la ASP, alisema kuwa wachimba madini wengine sita waliuawa kwa kukatwa vichwa na waasi wa kundi la CODECO.

 

Raia wengine watatu waliauwa katika shambulio lililofanywa na ADF na waasi usiku wa jumamosi katika jimbo la Kivu kaskazini mwa nchi hiyo, Congo inakabiliwa na makundi ya waasi ambao wamekuwa na kasumba ya kuwashambulia raia mara kwa mara.

 

Imeandikwa na:Oswald Mwesiga kwa msaada wa kimitandao.

Leave A Reply