Zifahamu Nchi Zenye Watu Wengi Zaidi Duniani, Tanzania Imo

HAISHANGAZI sana kuona kuwa nchi kubwa zaidi ulimwenguni ndio nchi zinazoongoza kwa idadi ya watu wengi zaidi duniani, mataifa kama Uchina na India, nchi zote mbili sasa zina idadi ya zaidi ya bilioni moja ya idadi ya watu.
Marekani inashika nafasi ya tatu ikiwa na wakazi zaidi ya milioni 335. Nchi za BRIC (Brazil, Russia, India na China), kwa ujumla zinazochukuliwa kuwa nchi nne kuu zinazoinukia kiuchumi ambazo zinazotarajiwa kutawala ulimwengu kiuchumi kwa miaka ijayo na zote zimo katika nchi kumi za juu zilizo na watu wengi zaidi, ikionyesha umuhimu wa ukubwa wa watu wao ukiendana kabisa na ukuaji wao wa kiuchumi yaani kuna balansi kubwa kati ya uchumi wao na wingi wa watu wao.

Kwa mujibu wa jarida la World of Statistics Mataifa matano yanatajwa kuwa na utofauti mkubwa kati ya wingi wa watu na ukuaji wa uchumi wao, (yaani, ambayo hayijafikia kiwango cha juu cha ukuaji wa viwanda kulingana na idadi ya watu wao) Mataifa hayo yapo katika orodha ya nchi 10 zenye watu wengi zaidi ingawa kwenye mataifa kama Urusi, Brazil, China na Marekani kwa ujumla mataifa hayo yana watu wengi lakini ynakuwa sana kiuchumi.
Mataifa hayo kiuchumi hayajakuwa sana lakini yana watu wengi sana kitu kinachotajwa kuwa wingi wa watu haujaendana na ukuaji wa uchumi katika mataifa yao, mataifa hayo ni Indonesia, Nigeria, Bangladesh, Pakistan na Mexico.
Zifahamu nchi hizo 10 zenye watu wengi zaidi duniani.
- China 1,425,867,569
- India 1,419,686,787
- United States 338,699,208
- Indonesia 275,959,684
- Pakistan 237,016,786
- Nigeria 219,894,398
- Brazil 215,566,694
- Bangladesh 171,646,703
- Russia 144,703,383
- Mexico 127,752,687
- Japan 123,782,579
- Ethiopia 124,186,426
- Philippines 116,021,326
- Egypt 111,434,166
- DR Congo 99,836,954
- Vietnam 98,365,332
- Iran 88,702,753
- Turkey 85,470,440
- Germany 83,340,333
- Thailand 71,726,445
- United Kingdom 67,568,334
- Tanzania 65,993,926
- France 64,660,772
- South Africa 60,021,855
- Italy 58,995,007
- Myanmar 54,283,725
- Kenya 54,300,735
- Colombia 51,918,099
- South Korea 51,808,906
- Spain 47,549,645
- Uganda 47,594,242
- Sudan 47,191,527
- Argentina 45,572,748
- Algeria 45,089,562
- Iraq 44,755,103
- Afghanistan 41,412,817

