The House of Favourite Newspapers

Etihad Yatunukiwa Hadhi ya Nyota Tano

1 Wafanyakazi wa ndani ya ndege za Etihad, wakiwa na Peter Baumgartner na Edward Plaisted.
2
Edward Plaisted (wa tano toka kushoto) kutoka Skytrax akiwakilisha wafanyakazi wa Etihad akiwa na hati ya uthibitisho wa hadhi ya nyota tano mjini Abudhabi.

==>Shirika la Ndege la Etihad limetambuliwa kuwa na ubora wa huduma za anga
==>Wakaguzi wapongeza wafanyakazi wa Etihad kwa huduma katika madaraja mbalimbali na             uanzishwaji wa vituo vya kuhudumia ndege

Etihad imepokea hati ya uthibitisho wa kuwa na hadhi ya nyota tano, kutoka kwa taasisi ya Skytrax ambayo inajihusisha na utafiti wa ubora wa huduma za anga Uingereza.

Hadhi hiyo inatokana na ukaguzi wa huduma za anga uliofanyika kwa miezi mitatu. Etihad ilitangazwa kutunukiwa hadhi hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye Chuo cha Uvumbuzi kinachomilikiwa na shirika hilo mjini Abudhabi.

Hadhi ya Nyota tano kwa mashirika ya ndege hutolewa na Skytrax ili kuthibitisha ubora wa juu katika huduma za anga kwa mashirika mbalimbali.

Vigezo vinavyozingatiwa katika utoaji wa hadhi hiyo ni pamoja na mpangilio wa ukaaji kwa abiria, usafi ndani ya ndege, burudani na huduma ya chakula.

Ofisa Mtendaji mkuu wa Etihad, Peter Baumgartner amesema, “Hadhi hii ni ishara ya matunda ya juhudi zetu za siku nyingi katika ukuaji wa huduma zetu za anga. Shirika letu limekuwa likizikabiri changamoto zinazojitokeza katika huduma za anga kwa kuboresha huduma ili kulifanya kuwa mfano wa kuigwa duniani kote.

“Jambo hili limewezekana kwa msaada mkubwa wa wafanyakazi wetu kuanzia nje mpaka ndani ya ndege, ambao wana mioyo ya kujituma na mapenzi kwa Shirika la Etihad.

Katika ukaguzi wa kina uliofanyika, wafanyakazi wetu pia wamepongezwa kwa kazi wanazozifanya. Watafiti pia wamefurahishwa na jinsi huduma zinavyotolewa, hasa kwa kuzingatia nidhamu ya kumhudumia mteja”.

Ofisa Mtendaji mkuu wa Skytrax Edward Plaisted amesema, “Etihad inaendelea kuongoza katika biashara ya huduma za anga. Kupewa hadhi ya nyota tano ni uthibitisho wa ubora wa juu katika huduma zetu. Katika kuonesha ubunifu, Etihad imeendelea kufanya mapinduzi katika huduma za anga kwa kuitambulisha ndege aina ya Airbus A380 na Boeing 787.

Ukarimu na nidhamu ya wafanyakazi wa Etihad kuanzia nje mpaka ndani ya ndege, unatokana na mwongozo wa Tamaduni za Kiarabu zinazo waongoza. Shirika pia limeajiri wafanyakazi wa jamii ya Savoy kutoka Uingereza, ambao wanahudumia wageni wa vyumbani katika ndege ya Airbus A380. Miongoni mwa wafanyakazi hao ni wapishi, walezi wa watoto na wahudumu wa vinywaji katika madaraja mbalimbali.

Etihad imepokea tuzo mbalimbali za Skytrax kutokana na huduma za daraja la kwanza na daraja la kawaida. Hivi karibuni Etihad ilipokea tuzo ya Shirika lenye daraja la kwanza lililo bora katika usafiri wa anga hasa katika huduma za chakula, pamoja na kushinda tuzo ya mwaka ya Mashirika ya ndege iliyotolewa mwezi Julai 2016, huko Farnborough. Tuzo hiyo imetokana na mpangilio mzuri wa ukaaji wa abiria katika Airbus A380.

Wakaguzi wameshuhudia ubora wa huduma za chakula katika daraja la kwanza zilizo sheheni ubunifu na ufundi katika maandalizi.

Ndege za Airbus A380 na Boeing 787 zimesheheni burudani na tekinolojia zinazokidhi mahitaji wakati wa safari.

Wakaguzi pia wamevutiwa na bidhaa mpya kama vile mito ya kupumzikia katika viti, runinga na sehemu za kuchajia ambazo zipo katika daraja la kati.

Nje ya Ndege, Etihad inaendesha jumla ya vituo 15 kwajili ya kuhudumia wateja wa anga, ikiwamo kilichopo Abudhabi.
Vituo vitatu katika temino ya kwanza na ya tatu, katika miji ya Frankfurt, London, Manchester, Dublin,Paris, Washington D.C, NewYork JFK, Sydney, Melbourne na Los Angeles

Vituo hivyo vinatoa huduma za Hoteli na watu binafsi. Pia kuna huduma za burudani na mapumziko.

Comments are closed.