The House of Favourite Newspapers

Majivu ya Mwili wa Fidel Castro Yazikwa Santiago, Cuba

_92826498_fidelasshesSANTIAGO, CUBA: Majivu ya aliyekuwa rais wa Cuba, Fidel Castro yamezikwa katika kiunga cha makaburi mjini Santiago, na hivyo kumaliza siku tisa za maombolezo ya kitaifa nchini humo.

Familia na wageni wachache walialikwa katika shughuli hiyo ya faragha, iliyofanywa karibu na makumbusho ya shujaa wa uhuru wa Cuba, Jose Marti.

Mbali na hivyo, rais wa Cuba, Raul Castro jana alieleza kuwa, serikali yake imepitisha sheria itakayozuia jina la Fidel Castro kutumika kama jina la mtaa au barabara ikiwa ni maagizo aliyotoa enzi za uhai wake.

Mbele ya mhadhara mkubwa mjini Santiago, alisema Fidel Castro hakutaka kufanywa kama kiongozi wa madhehebu.

halotel-strip-1-1

Comments are closed.