The House of Favourite Newspapers

Watu 259 Waliofungwa Minyororo Waokolewa Msikitini

 

JESHI la Polisi nchini Nigeria imewaokoa watu 259 kutoka katika kituo kisichokubalika kisheria kilichopo ndani ya Msikiti katika Mji wa Ibadan, jimbo la Oyo, Kusini Magharibi mwa nchi hiyo huku wengi wao wakiwa wamefungwa kwa minyororo.

 

Katika kipindi cha nyuma, zaidi ya watu 1,000 wameokolewa kutoka kwenye vituo vya kidini ambako mara kwa mara watu wamekuwa wakishikiliwa katika hali mbaya.

 

Wazazi wakiwapeleka wakiwatuma watoto wanaowasumbua kitabia na vijana wanaoaminiwa kuwa na uraibu wa madawa ya kulevya au wale waliopatikana na makosa madogo katika vituo vya Quran vya kurekebisha tabia.

Maofisa wamevifananisha vituo hivyo na vituo vya ukatili ambapo watu wanafungwa minyororo, kufungwa pamoja na kufanyiwa dhuluma.

 

Waliotekwa waliachiliwa Jumatatu jioni baada ya polisi kupewa taarifa na kijana mwenye umri wa maika 17 ambaye alikuwa ametoroka kutoka katika mahabusu nyingine katika eneo hilo.

 

Mmiliki wa mahabusu hiyo na watu wengine wanane wamekamatwa , limeripoti gazeti la Punch nchini humo.

Kamishna wa polisi wa jimbo hilo Bwana Shina Olukolu alinukuliwa akisema kwamba baadhi ya waathriwa wa utekaji huo wamesema wamekuwa wakishikiliwa kwa miaka kadhaa.

 

Hali katika msikiti huo ilikuwa ni mbaya kwa binadamu kuishi na baadhi ya vifo vya waathirika vilivyotokea havikuripotiwa, alinukuliwa akisema.

 

Huu ni mojawapo ya uvamizi wa wa hivi karibuni wa vituo vinavyoitwa ”vituo vya kiurekebisha tabia” nchini Nigeria ambamo watu wanashikiliwa katika hali mbaya mkiwemo kufungwa na minyororo.

 

Wengi husajiliwa kwenye taasisi hizo na ndugu zao ili kupata usaidizi wa kiroho na kurekebisha tabia kwa wanaotumia madawa ya kulevya.

Comments are closed.