The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Italia, Matteo Renzi Ajiuzulu

Foto Roberto Monaldo / LaPresse 13-03-2014 Roma Politica Rai1 - Trasmissione tv "Porta a Porta" Nella foto Matteo Renzi Photo Roberto Monaldo / LaPresse 13-03-2014 Rome (Italy) Tv program "Porta a Porta" In the photo Matteo Renzi

Waziri Mkuu wa Italia, Matteo Renzi amejiuzulu baada ya kukubali kushindwa katika kura ya maamuzi kuhusu marekebisho ya katiba nchini humo.

Akihutubia wanahabari jana usiku, kiongozi huyo alisema anakubali lawama kutokana na matokeo hayo, na kwamba kambi ya HAPANA, ambayo ilipinga mageuzi hayo, sasa inafaa kutoa mapendekezo ya mwelekeo kutoka sasa.

Baada ya sehemu kubwa ya kura kuhesabiwa, kambi ya HAPANA inaongoza kwa 60% dhidi ya 40% za NDIYO.

Waliojitokeza kupiga kura walikuwa takriban 70% ya wapiga kura wote waliojiandikisha, jambo linalotazamwa na wengi kama ishara yao kuonesha kutoridhishwa kwao na waziri mkuu huyo.

“Kila la heri kwetu sote,” Bw. Renzi aliwaambia wanahabari.

Alieleza kuwa ataitisha mkutano wa baraza la mawaziri baadaye leo kisha atawasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa rais wa Italia.

halotel-strip-1-1MZEE WA MIAKA 76 ALEYETANAGAZA KUTAFUTA MKE “FULL EXLUSIVE INTERVIEW”

Comments are closed.