TCRA Yawatahadharisha Watumiaji wa Kompyuta juu ya Kirusi Kiitwacho WANNACRY

Shambulizi la kihalifu mitandaoni lililotendeka kupitia vifaa vinavyoaminika kuibwa kutoka kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri mashirika tofauti duniani.

Kirusi cha WannaCry baada ya kushambulia kompyuta.

Kampuni ya kulinda uhalifu wa mitandao Avast, imesema kuwa imeona kesi 75,000 za programu zinazotumika kufanya uhalifu mtandaoni inayojulikana kama ‘WannaCry’ duniani.
Kuna ripoti za maambukizi katika mataifa 99 ikiwemo Urusi.
Kati ya mashirika yalioathirika zaidi ni shirika la huduma za afya nchini Uingereza na Uskochi.
Programu hiyo ilisambaa kwa kasi siku ya Ijumaa ambapo ilitaka malipo ya dola 300 ili kufungua faili ilizokuwa imeziteka nyara katika kompyuta. Siku nzima, mataifa ya Ulaya yaliripoti maambukizi hayo.

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment