The House of Favourite Newspapers

Omog: Huyu Okwi ni Mashine

0
Emmanuel Okwi.

KIKOSI cha Simba kilirejea nchini juzi Jumamosi, kikitokea Afrika Kusini kilipokuwa kimepiga kambi kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara 2017/18, pia Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Simba ambaye ni raia wa Cameroon, Joseph Omog amemmwagia sifa za pekee mshambuliaji wake mpya, Mganda, Emmanuel Okwi kwa kusema kuwa wamelamba dume, kwani mchezaji huyo ni mashine uwanjani.

Akizungumza na Championi Jumatatu muda mfupi tu baada ya kutua nchini, Omog alisema katika muda mfupi ambao amekaa na Okwi katikia kikosi chake amegundua ana mambo mengi ambayo ni tofauti kabisa na wachezaji wengine.

 

“Nashukuru Mungu tumerejea nchini salama lakini pia kambi yetu ilikuwa ni nzuri sana na imetujenga vilivyo kwa ajili ya msimu ujao na imeniwezesha kuwajua vizuri baadhi ya wachezaji waliosajiliwa hivi karibuni.

“Hata hivyo, nimevutiwa sana na Okwi, kwani katika muda mfupi niliokaa naye kambini nimeweza kugundua mambo mengi kutoka kwake ambayo ni tofauti kabisa na wachezaji wengine.

 

“Anajua majukumu yake anapokuwa uwanjani, pia nje ya uwanja anajua afanye nini, hakika atakuwa msaada mkubwa kwetu safari hii katika harakati zetu za kuwania ubingwa wa ligi kuu ikiwa ni pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika,” alisema Omog na kuongeza:

“Kwa yeyote anayetaka kuthibitisha haya ninayoyasema aje uwanjani siku ya Jumanne (kesho) tutakapopambana na Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.”

 

Sweetbert Lukonge | Dar es Salaam

 

Leave A Reply