The House of Favourite Newspapers

Dudubaya: Natamani Nikamue Tena Fiesta

0
Msanii wa kitambo kwenye Bongo Fleva, Dudubaya.

MSANII wa kitambo kwenye Bongo Fleva, Dudubaya amefunguka kuwa anatamani kuendelea kuonyesha makeke yake kwenye Tamasha la Fiesta linaloendelea kwenye mikoa tofauti baada ya hivi karibuni kupanda jukwaani wakati tamasha hilo likiwa mkoani Mwanza.

 

Dudubaya alipata nafasi ya kupanda jukwaa la Fiesta Mwan­za baada ya kuitwa jukwaani na msanii Bernard Paul ‘Ben Pol’.

 

Akizungumza na Cham­pioni Jumamosi, Dudubaya aliyetamba na ngoma kibao kama Mpenzi, Nakupenda Tu na nyinginezo kibao amesema anatamani kuen­delea kuonyesha makeke yake baada ya kupata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wakati akikamua kwenye tamasha hilo.

 

 

“Kiukweli natam­ani nipate tena nafa­si ya kupanda jukwaani kwenye Fiesta kwa sababu ya mapokeo ya aina yake niliyoyapata waka­ti nikiimba ngoma zangu am­bazo ziliwakosha watu wengi akiwemo mkuu wa mkoa wa hapa,” alisema Dudu Baya.

STORI: SAID ALLY | CHAMPIONI

Leave A Reply