The House of Social Media
gunners X

Tuyisenge Afunguka Kutua Yanga SC

0

 

HATIMAYE mshambuliaji wa APR ya nchini Rwanda, Jacques Tuyisenge, amefungukia dili lake la kujiunga na Yanga ambayo amekuwa akihusishwa nayo kwa muda mrefu.

 

Tuyisenge mwenye uraia wa Rwanda, aliwahi kutamba katika kikosi cha Gor Mahia akiwa sambamba na nyota wa sasa wa Simba, Meddie Kagere, Francis Kahata na Joash Onyango.

 

Akizungumza na Spoti Xtra juu ya kuhitajika ndani ya Yanga, mshambuliaji huyo alisema: “Kwa sasa mimi ni mchezaji wa APR, siruhusiwi kufanya mazungumzo yoyote yanayohusu masuala ya usajili kwani kila kitu kinachohusu usajili wangu kinasimamiwa na meneja wangu Eto Mupenz.”

 

Spoti Xtra lilipomtafuta meneja wa mchezaji huyo, alisema kuwa bado hajapokea ofa yoyote kutoka Yanga inayomuhusu mshambuliaji huyo ambaye bado ana mkataba na APR.“

 

Tuyisenge bado ana mkataba wa kuendelea kuitumikia APR na kuhusu kutakiwa na Yanga bado sijapokea ofa yao na ambacho kinaongelewa kwa sasa ni tetesi tu, mazungumzo kamili hakuna,” alisema meneja huyo.

STORI: MARCO MZUMBE NA IBRAHIM MUSSA, DAR

Leave A Reply