The House of Social Media
gunners X

Mkurugenzi NIDA na Wenzake Wakutwa na Hatia

0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewakuta na kesi ya kujibu, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu na wenzake wanne na wataanza kujitetea, Agosti 25 na 26, mwaka huu.

 

Uamuzi huo umetolewa leo, Agosti 11, mwaka huu na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili uamuzi kama washtakiwa wana kesi ya kujibu ama laa.

 

Maimu na wenzake, wanakabiliwa na mashtaka 55 yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh 1.175 Bilioni. Hakimu Chaungu alisema kuwa amepitia mashtaka yote na vielelezo vyote, ameridhika kuwa washtakiwa wote wana kesi ya kujibu, hivyo watatakiwa kujitetea.

 

Washtakiwa wamedai kuwa watajitetea kwa kiapo na watakuwa na mashahidi na vielelezo. Hakimu Chaungu baada ya kueelaza hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 25 na 26, 2021 ambapo washtakiwa wataanza kujitetea.

 

Mbali na Maimu, washtakiwa wengine ni Ofisa Usafirishaji wa NIDA, George Ntalima; Meneja Biashara wa NIDA, Avelin Momburi; Xavery Silverius maarufu kama Silverius Kayombo na Mkurugenzi wa Sheria NIDA, Sabina Raymond.


Leave A Reply