Watano Wafariki Ajali ya Helikopta Juu ya Mlima Kilimanjaro

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kupitia Kamanda wa Polisi (RPC), Simon Maigwa, limethibitisha vifo vya watu watano waliopoteza maisha katika ajali ya helikopta iliyokuwa imekwenda kuwachukua watalii katika Mlima Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), helikopta hiyo ilianguka kwenye eneo la barafu, juu ya Mlima Kilimanjaro, majira ya saa 11:30 jioni, Desemba 24, 2025.

TANAPA imeeleza kuwa helikopta hiyo, aina ya Airbus AS350 B3 inayomilikiwa na Kampuni ya KilimediAIR, ilikuwa na watu watano:
— Watalii wawili raia wa Jamhuri ya Czech,
— Raia wawili wa Tanzania (muongoza watalii na daktari),
— Rubani ambaye ni raia wa Zimbabwe.
Chanzo cha ajali bado hakijabainika. TANAPA, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Usalama wa Anga, inaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini kilichotokea.


