CHADEMA Yatoa Tamko Upotoshaji Michango kwa Tundu Lissu

DAR-Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kumekuwepo taarifa za upotoshaji zinazosambazwa na watu wasiokitakia mema chama hicho zikiwahusisha viongozi wa chama na kashfa zinazohusisha madai ya michango iliyoendeshwa hivi karibuni mtandaoni ili kumchangia Mwenyekiti wa chama,Tundu Lissu.


