Kiredio Avuna Milioni 20+ Kupitia Project ya Mapenzi Mubashara

Katika kipindi hiki ambacho maudhui ya mitandaoni yamekuwa ajira kamili kwa vijana wengi, mtangazaji na muandaaji wa maudhui Vicent Njau maarufu Kiredio ameonyesha kuwa ubunifu unaweza kugeuka kuwa pesa halisi.
Kupitia kampeni yake ya kimapenzi iliyopewa jina la Mapenzi Mubashara, Kiredio alikuja na wazo la kipekee la kuandaa project maalum ya siku 14 mfululizo, akishirikisha maudhui yanayohusu mapenzi, mahusiano na maisha halisi ya kimahaba yaliyowavutia mashabiki wake kwa kiasi kikubwa.
Project hiyo haikuishia kuwa burudani tu bali imegeuka kuwa chanzo kikubwa cha mapato.
Kwa mujibu wa Kiredio mwenyewe, anadai kuwa ndani ya siku hizo 14 pekee, ameweza kuingiza zaidi ya Shilingi Milioni 20 za Kitanzania, kupitia matangazo, promosheni za bidhaa (brand deals), ushirikiano wa kibiashara pamoja na nguvu ya ushawishi alionao kwa wafuasi wake.


