The House of Favourite Newspapers

Chid Benz: Hata Mama Yangu Haniulizi Kuhusu Madawa

Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ akiwa mikononi mwa polisi.

 

JANGA la matumizi ya madawa ya kulevya hapa nchini limekuwa kubwa siku hadi siku na hata duniani kwa jumla, watu mbalimbali wamekuwa wakiathirika na madawa hayo hususani wasanii ambao baadhi yao wamepotea katika soko la muziki kutokana na kujiingiza katika matumizi hayo.

 

Miongoni mwa wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya ambao wameathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na matumizi hayo ni Rashid Makwiro ‘Chid Benz’.

 

Msanii huyu ni muhanga mkubwa kutokana na kushindwa kujimudu kwa sasa katika muziki kutokana na athari alizozipata za madawa.

Chid kabla ya kujiingiza kwenye matumizi hayo, alifanikiwa kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa hapa nchini na kufanya vyema katika gemu la muziki ambapo alitambuliwa zaidi kupitia wimbo wake wa Dar es Salam Stand Up ambao ulipokelewa vyema na mashabiki wake.

Chid alikuwa akisifika kwa sauti nzuri yenye mvuto katika nyimbo zake kadhaa alizowahi kuimba hali ambayo iliwavutia kwa kiasi kikubwa wasanii wenzake kufanya naye kolabo.

Championi Ijumaa inakuchambulia jinsi msanii huyo alivyoathirika kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya na maendeleo yake kwa sasa.

 

Ikumbukwe kuwa, umaarufu wa Chid Benz ulipotea ghafla baada ya kuanza kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya zaidi ya miaka mitatu nyuma hali iliyoathiri mfumo wake mzima wa maendeleo pamoja na afya kwa jumla.

 

Chid aliwahi kukiri kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya kupitia kituo kimoja cha redio hapa nchini katika siku za nyuma kwa kuomba msaada kwa ajili ya kujiondoa katika matumizi hayo jambo ambalo lilifanyika baada ya Babu Tale na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ kujitolea kumsaidia kwa kumpeleka katika Sober House ya Bagamoyo inayoitwa Life and Hope ambapo alikaa kidogo kabla ya kurejea uraiani na kuimba kibao cha Chuma ambacho hakikuweza kutamba vilivyo.

Sikio la kufa halisikii dawa, hivyo ndivyo unavyoweza kusema, kutokana na msanii huyo kurejea tena katika matumizi ya madawa ya kulevya kwa mara nyingine na kusababisha apelekwe katika soba ya Iringa alikokaa kwa siku kadhaa kabla ya kurejea tena uraiani na kuendelea na matumizi yake kama kawaida.

 

Mwishoni mwa mwaka jana, Chid alikamatwa na madawa ya kulevya mkoani Dodoma na jeshi la polisi baadaye lilimuachia.

Lakini hali inaendela kuonekana haikuwa sawa kwa upande wake kutokana na mara kadhaa kudaiwa kukutwa katika vijiwe vya matumizi ya madawa hayo na hata sauti yake imeonekana kubadilika na sio ile ambayo imezoeleka

ya kulevya na hali yake kwa sasa ambapo hapa anasema: “Sitaki kuongelea kuhusu madawa ya kulevya kwa sasa, hata mama yangu mzazi haniulizi swali hilo kipindi hiki kwa sababu sitaki kusikia.

 

“Hata aje mtangazaji kutoka BBC siwezi kumjibu swali hilo, kila siku unataka mimi niongelee kuhusu madawa ya kulevya, mambo ya madawa ya kulevya ni mabaya.

“Naomba mniache mkae kimya kama mnavyokaa kimya kwa wasanii wengine ambao wanatumia madawa lakini hamuwaulizi.

“Kama navuta ama sivuti niacheni mwenyewe. Nipo tayari kutoa ushirikiano katika kazi ya muziki, kwa sasa ninaendelea na kazi yangu ya muziki, nawaandalia mashabiki wangu nyimbo ambazo zitakwenda na wakati uliopo.”

MAKALA, KHADIJA MNGWAI, CHAMPIONI IJUMAA

Comments are closed.