The House of Favourite Newspapers

Spotipesa Super Cup 2018 Kufanyika Kenya

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SpotiPesa Tanzania, Tarimba Abbas, akiongea jambo wakati wa uzinduzi huo makao makuu ya ofisi zao Masaki jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, akizungumza namna timu yake ilivyojipanga kushiriki mashindano hayo.
Mjumbe wa Kamati ya Mashindano wa Simba, Said Tully, akielezea namna Simba itakavyopambana kwenye michuano hiyo.
Abbas (mwenye suti katikati) akiwa na viongozi wa timu zitakazoshiriki mashindano hayo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo wakiwajibika.

 

AWAMU ya pili ya mashindano ya SpotiPesa Super Cup yanayotarajiwa kuanza kurindima Juni 3 hadi 10 mwaka huu katika Uwanja wa Kimataifa wa Moi uliopo Kasarani Nairobi Kenya, yamezinduliwa rasmi na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SpotiPesa Tanzania, Tarimba Abbas, makao makuu ya ofisi zao Masaki jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Abbas alisema mashindano ya mwaka huu yatashirikisha vilabu vinane ambapo klabu nne zitatoka nchini Tanzania na nne Kenya.

 

Klabu hizo ni Simba, Yanga, Singida United na JKU zote za Tanzania, wakati Kenya ni Gor Mahia, AFC Leopard, Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboys.

 

“Matayarisho ya mwaka huu yamefanyika mapema na ukiangalia muda ambao timu tumezipa taarifa hadi leo tunazindua ni karibia mwaka mzima umepita hivyo basi hakuna sababu yoyote ya kuzifanya timu zetu za Tanzania zifanye vibaya kwani tuna imani kila timu itakuwa imejiandaa vya kutosha.

 

“Kama nilivyosema awali,  michuano hii itakutanisha timu nane kwa maana ya nne kutoka Tanzania na nne zingine za Kenya, ambapo mshindi kati yao atapata nafasi ya kucheza na Everton, mchezo utakaopigwa nchini Uingereza.

 

“Timu zitakazoingia robo fainali ya mashindano hayo zitapata dola za Marekani 2,500, atakayeingia nafasi ya nne atapata dola 5,000,wakati nafasi ya tatu na wa pili watapata dola 7,500 na dola 10,000 kila mmoja, lakini timu itakayoibuka na ushindi itachukua dola 300,00 huku ikipata tiketi ya kwenda Uingereza kupapambana na Everton,” alisema Abbas.

(PICHA/HABARI: MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS)

SPOTI HAUSI: Kigogo DAR Aipandisha Mshikamano Ligi Kuu VPL

 

Comments are closed.