The House of Favourite Newspapers

Aunt Ezekiel Atoa Shukurani Kanisani

Aunt Ezekiel Grayson

STAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson ametoa shukurani zake kanisani baada ya kuugua mno na kupoteza fahamu kwa siku mbili kiasi cha kuchungulia kaburi. Aunt aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa ishu hiyo aliifanya wiki iliyopita katika Kanisa Katoliki la Kisarawe mkoani Pwani, mahali ambapo alikulia.

 

Alisema kuwa, aliamua kufanya hivyo kwa sababu alipokuwa akiumwa hakujua kama ataweza kuinuka tena na kuzungumza kama zamani kwani alishakata tamaa, lakini Mungu akamponya hivyo hana budi kumrudishia shukurani.

 

“Mungu alinitendea makuu kwa kuniinua tena kitandani na kuweza hata kuzungumza hivyo sina budi kumshukuru,” alisema Aunt.

Comments are closed.