The House of Favourite Newspapers

Mwambusi Apewa Miaka Miwili Azam FC

Kocha wa zamani wa Yanga, Juma Mwambusi.

KLABU ya Azam FC imeendelea na maandalizi yake ya kujiweka sawa na msimu ujao wa 2018/19 ambapo jana Jumanne iliingia makubaliano na aliyekuwa kocha wa zamani wa Yanga, Juma Mwambusi.

 

Azam imeingia makubaliano na kocha huyo na kumpa mkataba wa miaka miwili huku akiwa kocha msaidizi wa Mholanzi Hans van Pluijm ambaye ndiye kocha mkuu.

 

Azam imemrudisha tena kocha huyo uwanjani baada ya kujiweka kando tangu msimu uliopita ambapo mara ya mwisho alikuwa na kikosi cha Yanga. Meneja wa Azam, Phillip Alando ameliambia

 

Championi Jumatano, kuwa wamemalizana na Mwambusi na tayari alishaanza kazi ndani ya kikosi hicho tangu jana Jumanne mara baada ya kusaini mkataba.

 

“Kweli tumelizana na kocha Juma Mwambusi na ameingia mkataba wa miaka miwili na sisi, tayari ameshaanza kazi mara moja tu baada ya kusaini mkataba huo.

 

“Yeye atakuwa kocha msaidizi akisaidiana na wenzake, Hans Pluijm, Idd Cheche na Idd Abubakar kocha wa makipa ambao wao ndiyo watakuwa benchi letu la ufundi,” alisema Alando.

Comments are closed.