The House of Favourite Newspapers

Aslay Ndani Ya Penzi Zito na Mrembo Mwingine

STAA wa muziki wa Bongo Fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Nibebe’,  Aslay Isihaka,  ameweka wazi penzi lake zito na mrembo ambaye ni muigizaji wa Bongo Movie, Diana Kimary.

Wiki chache zilizopita Aslay alithibitisha kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Tessy Chocolate, ambaye pia ni mama wa mtoto wake mmoja wa kike anayeitwa Moza.

Aslay na Tessy hawakuweka wazi sababu za kuachana lakini kila mmoja alisisitiza wameachana kwa wema na hawana chuki baina yao.

Jana Aslay amemuanika rasmi Diana kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amemposti mara mbili.
Kwenye picha hizo Aslay alisindikiza kwa maneno kama “Mashallah” na “Sasa ndio nini Mke wangu”.

Comments are closed.