The House of Favourite Newspapers

Radi, Mvua Kubwa Zavunja Mazoezi Ya Simba Uturuki

MVUA kubwa yenye ukungu uliopita kiasi, radi na ngurumo za kutisha, jana vilisitisha mazoezi ya mab­ingwa wa Tanzania, Simba.

 

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems alilazimika kusitisha mazoezi na kuondoa kikosi chake uwanja­ni wakati wa mazoezi ya asubuhi kutokana na mvua hiyo kubwa.

 

Hali ya hewa ilianza kubadilika taratibu wakati Simba wakijifua na ukungu ukaanza kutanda uki­washangaza wachezaji na benchi la ufundi.

 

Lakini ghafla, wakati mazoezi yakiendelea mvua kubwa ilianza kunyesha na kusababisha kocha huyo Mbelgiji kusitisha mazoezi.

 

Kocha mpya wa viungo wa Simba, Adel Zrane alishindwa kuendelea na kazi yake ikiwa ndiyo siku ya kwanza ameanza kazi.

 

Aussems ali­waambia wache­zaji wake, mazoezi ya jana jioni wangeangalia hali ya hewa. Kama bado ingeen­delea kutishia amani, basi ratiba ingebadilika na kuwa gym kwa kuwa katika eneo la Kartepe gym iko katika vyumba vilivyo chini ya ardhi yani underground.

Comments are closed.