The House of Favourite Newspapers

NAFASI ZA KAZI 4 KUTOKA RITA, MWISHO KUOMBA AGOSTI 17

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niamba ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 4 kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.

 

WAKALA WA USAJILI, UFILISI NA UDHAMINI (RITA)

RITA ni Wakala wa Serikali ulianzishwa chini ya Sheria ya Bunge Na.30 ya Mwaka 1997 kufuatia Tangazo la Serikali Na. 397 ya tarehe 2/12/2005. RITA ina jukumu la kuhakikisha ufanisi katika usimamizi wa taarifa yaMatukio Muhimu ya Binadamu na Huduma za Ufilisi na Udhamini Tanzania. Wakala unatafuta:-

1.2 Afisa Usajili Msaidizi Daraja la II Nafasi (4)

1.3Majukumu ya kazi ya Afisa Usajili Msaidizi Daraja la II
i.Kusajili Ndoa, Vizazi na Vifo na Muungano wa Wadhamini na kutunza kumbukumbu
zake.
ii.Kukusanya ada za Ndoa, Vizazi na Vifo na Muungano wa Wadhamini.
iii.Kutayarisha Fahirisi (Index) za Ndoa, Vizazi na Vifo kwa wilaya na mikoa.
iv.Kutayarisha matangazo yahusuyo shughuli za mirathi yan
ayotolewa katika gazeti la Serikali na hati za malipo mbalimbali kuhusu mirathi.
v.Kutunza magazeti ya Serikali, nyongeza za Sheria (Acts Supplements).
vi.Kutunza Ratiba za kesi za Mahakamani zinazohusu mirathi (Court Diary) na
kuwakumbusha Mawakili wa Serikali wanaohusika.
vii.Kupokea taarifa na kufanya upekuzi.
viii.Kuwaelekeza wananchi kuhusu utaratibu wa kuendesha mirathi

BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI

Comments are closed.