The House of Favourite Newspapers

NAIBU WAZIRI TAMISEMI AFUNGUA KONGAMANO LA 10 LA WADAU WA ELIMU

Naibu wa Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Josephat Kandege  akizungumza kwenye kongamano la 10 kwa wadau wa elimu kujadili ufundishaji wa umahiri na ujuzi. 
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao (wa pili kulia) akizungumza kwenye kongamano hilo.
Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Dodoma, Tumsifu Mwasamale (katikati) akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dodoma akizungumza kwenye kongamano la 10 kwa wadau wa elimu.
Mkurugenzi wa Right To Play Tanzania, Josephine Mukakausa (kulia) akizungumza kwenye kongamano hilo.
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao (katikati) akimkabidhi baadhi ya machapisho ya mtandao huo Naibu wa Waziri, Josephat Kandege (wa pili kulia).
Mwakilishi wa Right To Play (kulia) akimkabidhi baadhi ya machapisho ya taasisi hiyo Naibu wa Waziri,  Josephat Kandege.

 

 

NAIBU wa Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mh. Josephat Kandege leo amefungua kongamano la 10 kwa wadau wa elimu kujadili ufundishaji wa umahiri na ujuzi kwa wanafunzi ili uwasaidie kukabiliana na changamoto zinazowakabili kwa sasa.

 

 

Kongamano hilo lililoratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT) limefunguliwa jana Desemba 4, 2018 Jijini Dodoma na Mh. Kandege kwa niaba ya waziri wake huku akiwapongeza wadau hao kwa juhudi za kuendelea kuiboresha elimu, hivyo kuwahakikishia Serikali inasubiri kwa hamu mapendekezo ya kongamano ili iyafanyie kazi.

Programu Ofisa wa Right To Play Tanzania, Maria Mungi akiwasilisha mada kwa washiriki wa kongamano hilo juu ya namna michezo inavyoweza kutumika kufundishia wanafunzi masomo mbalimbali.

 

Alisema hapo nyuma ilifika kipindi vijana walikuwa wakifundishwa namna ya kujibu mitihani jambo ambalo limekuwa changamoto kijana huyo anapoingia mtaani na kukuta mambo tofauti. “Tunasema tunataka kufanya mapinduzi lazima hivyo lazima twende pamoja kama hivi na kuibuka na majibu,” alisema.

 

“Haya ambayo mnaenda kuyafanya kwa siku mbili hizi mnazokutana tunaamini kazi nzuri ambayo unaenda kuifanya inakwenda kuliokoa taifa la Tanzania kutoka katika hali ambayo watu wengi wamekuwa wakitilia mashaka juu ya elimu yetu…na sasa tunakwenda kuwa taifa litakalopigiwa mfano kwa ubora wa elimu.”

 

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao alisema wadau hao wamekutana kuangali uwajibikaji wa pamoja kwa wadau wote wa elimu utakao ibuka na ufundishaji wa umahiri na ujuzi.

 

“Lengo letu ni kujadiliana kuona tutawajibika vipi ili kuifanya elimu yetu iwe bora, inayowapa wanafunzi umahiri na ujuzi. Mwisho wa siku tutaangalia nani afanye nini katika hili ili kuleta mapinduzi ya kweli kwenye elimu yetu,” alisisitiza Bi. Sekwao.

 

 

Aidha alibainisha kwa sasa mwanafunzi wa kidato cha nne ambaye hajaendelea na masomo anakuwa nyumbani tu kutokana na kukosa ujuzi. “Njia pekee ya kuwasaidia wanafunzi kama hawa hasa kipindi hiki cha Tanzania ya viwanda ni kuwapa ujuzi wanafunzi wetu ili waweze kuwa chachu kuelekea kwenye sera ya sasa ya Tanzania ya viwanda”.

 

 

Naye Dk. Luka Mkonongwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, DUCE akiwasilisha mada kwa washiriki alisema kama yatafanyika mabadiliko kwenye mfumo wa elimu nchini yaani toka kuwapa wanafunzi maarifa na kwenda kujenga umahiri na ujuzi yapo mambo ya kuzingatia.

 

 

“kimsingi mapinduzi haya yana gharama zake, ni lazima kubadili mfumo mzima wa elimu na kuangalia upya. Lazima kuangalia suala la idadi ya wanafunzi na masomo tuliyonayo, kuangalia vifaa vya kufundishia na kujifunzia wanafunzi hao vipo vya kutosha,” aliongeza.

 

 

Pamoja na hayo alibainisha kuangaliwa vifaa vya kufundishia, bajeti inayopeleka kwenye elimu kama inatosha, kuangalia pia wadau wengine ushiriki wao, wazazi, asasi za kiraia na taasisi zingine zote zinawajibu gani kufanikisha. Alisema kuna haja ya kutulia na kufanya tafiti za kutosha kabla ya kufanya mabadiliko hayo kwa kushirikisha maoni ya wadau wote.

Comments are closed.