The House of Favourite Newspapers

Okwi Asepa Simba Na Mabegi Yote

Em­manuel Okwi

MSHAMBULIAJI wa Simba, Em­manuel Okwi, juzi Ju­manne, aliwashangaza wengi baada ya kuondoka nchini na kwenda kwao Uganda huku akibeba mabegi yake yote muhimu.

 

Okwi ambaye dili lake la kutua Kaizer Chief ya Afrika Kusini likionekana kuiva, aliwashanga wengi huku watu wakidai kwamba ndiyo safari imeiva.

 

Chanzo makini kutoka ndani ya Simba kimeliambia Spoti Xtra kuwa, juzi Jumanne Okwi alipewa ruhusa na kocha wake, Patrick Aussems kwenda Uganda kusherehekea Sikukuu ya Krismasi na familia yake, lakini alimtaka kurudi nchini mapema kuunga na wenzake.

 

Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kwamba, wakati Okwi anaondoka, alibeba mabegi yake yote muhimu jambo ambalo wengi walilitafsiri kwamba ameanza kuhamisha vitu vyake ili akiondoka moja kwa moja asipate shida.

“Okwi ameondoka kwenda kwao Uganda kusherehekea sikukuu na familia yake, ruhusu hiyo amepewa na Kocha Aussems, lakini amemtaka arudi Alhamisi (leo) ili awepo kwenye maandalizi ya mechi ya Jumapili dhidi ya Singida United.

 

“Lakini wakati anaondoka, aliwashtua wengi kutokana na kwamba amekusanya mabegi yake yote muhimu, bila shaka atakuwa ameanza kuhamisha kila kitu chake kabisa ili atakaporudi na akiruhusiwa kwenda Afrika Kusini awe hana vitu vingi vya kuhamisha,” kilisema chanzo hicho.

 

Hivi karibuni, Okwi aliliambia Spoti Xtra kuwa, dili lake la kutua Afrika Kusini lilikuwa limeiva, alichokuwa anasubiria ni ruhusa kutoka kwa viongozi wake wa Simba.

Comments are closed.