The House of Favourite Newspapers

Uchaguzi Waiponza Simba Congo

UNAWEZA kusema mambo ni magumu kidogo kwa kuwa wakati fulani Kocha Patrick Aussems alilazimika kufanya kazi zake kwenye ubalozi wa Tanzania nchini hapa. Hii inatokana na uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuamua kuzima mitambo inayorusha mtandao maarufu kama internet.

 

Uamuzi huo unatokana na masuala ya kiusalama nchini hapa kwa kuwa ulifanyika uchaguzi mkuu lakini hata baada ya kutangazwa kwa Felix Tshisekedi kuwa mshindi kumekuwa mapingamizi kadhaa na hasa lile la mgombea mwenzake, Martin Fayulu aliyeshika nafasi ya pili kuamua kufungua kesi akipinga.

 

Mambo kadhaa ambayo yanalazimisha kupatikana kupitia internet hayafanyiki sehemu zote za mjini. Katika ubalozi wa Tanzania, kuna mtandao hivyo kocha na maofisa wa Simba walifika mara kadhaa kufanya mambo yao muhimu.

Hata waandishi wa habari nao walijikuta katika wakati mgumu kutokana na hali hiyo iliyowalazimisha kushindwa kufanya kazi zao kwa wakati mwafaka.

 

Simba iko jijini hapa tayari kuwavaa AS Club Vita ambayo ni moja ya timu maarufu zaidi hapa Kinshasa na DR Congo kwa ujumla.

Hali ilivyo kuna utulivu ingawa gumzo la mechi hii limekuwa likipanda hasa kutokana na AS Vita Club kuanza kwa kupoteza dhidi ya Al Ahly na Simba
wakiwa wameanza kwa kukusanya pointi tatu dhidi ya JS Saoura ya Algeria.

Comments are closed.