The House of Favourite Newspapers

ACB YAJIDHATITI KUWAINUA WAJASILIAMALI WADOGO

 

Mkurugenzi  Mtendaji wa ACB, Augustine Akowuah akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Meneja Mkuu Kitengo cha Fedha wa Benki ya Akiba Commercial (ACB) Bertha Simon akielezea mikakati waliyojiwekea kwa mwaka 2019.

 

 

BENKI ya Akiba Commercial (ACB)   imejizatiti katika kuwainua wajasiliamali wadogo na wa kati kwa kuwapatia mikopo nafuu na ya muda mrefu ili kuwawezesha kujikwamua.

 

 

Akiba Commercial Bank ilimaliza nusu ya pili ya mwaka ulioishia Desemba 2018 kwa kupata faida ghafi yaani Pre-tax profit ya TZS 1.2 bilioni, ikiwa ni ukuaji wa asilimia 600 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kilichoishia Desemba 2017.

 

 

Ongezeko la faida lilitokana na ukuaji wa mikopo ,amabayo ilitolewa kwa wateja 13,200 wengi wakiwa ni wafanyabiashara wadogo na kati iliyofikia kiasi  cha TZS 80 bilioni.

 

 

Ubora wa mikopo hiyo ulikuwa mzuri kwenye kipindi hicho, kutokana na maboresho ya taratibu za utoaji wake.Wastani wa mikopo chechefu ulikuwa ni asilimia 0.7 hadi kufikia Desemba 2018.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi  Mtendaji wa ACB, Augustine Akowuah alisema kuwa”Ninafarijika sana na matokeo haya ya nusu ya pili ya mwaka jana; mizania ya malengo yetu tangu mwanzo wa mwaka yametusababisha kuwa na muelekeo mzuri wakati tukifunga mwaka.

 

Tunafurahi kwa sababu mikakati mingi tuliyojiwekea imeleta mabadiliko kwenye benki yetu kwa muda mrefu, japokuwa hali haikuwa nzuri mwanzo wa mwaka”.

 

“Katika kipindi cha mwaka 2018, akiba ilitekeleza mikakati ya kupunguza mikopo chechefu, kuimarisha makusanyo ya madeni sugu na utoaji wa mikopo mipya kwa kuzingatia ubora. Hatua tulizozichukua ikiwemo kubadilisha na kupitia majukumu na kazi zililenga zaidi kwenye kuimarisha hatari zinazotokana na ukopeshaji”. Alisema  Akowuah.

 

Matarajio ya benki kwa mwaka 2019 ni kuendelea kuwa na matokeo chanya, kwani tunalenga kujenga maendeleo chanya yaliyopatikana mwaka 2018 ikiwemo jukumu pekee la kusaidia wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs) nchini Tanzania kwa kutumia huduma bora za kifedha.

 

 

Akiba Commercial Bank ni benki ya kitanzania iliyoanzishwa miaka 20 iliyopita na inatoa huduma za kifedha kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, pamoja na watanzania kwa ujumla. Wateja 122, 000 wa benki wanapata huduma za kifedha kupitia mifumo ya kidijitali pamoja na mtandao wa matawi 18 yaliyopo kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mbeya, Moshi na Mwanza.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.