The House of Favourite Newspapers

Kagere Akataa Tuzo Simba SC

Meddie Kagere wa Simba.

MSHAMBULIAJI Mnyarwanda, Meddie Kagere wa Simba ameweka bayana kwamba ndani ya klabu hiyo na ligi kuu hataki tuzo ya aina yoyote kwa sababu anachokifanya ni kusaidia timu yake.

 

Kagere ndiye anayeongoza kwa mabao ndani ya Klabu ya Simba baada ya kufunga mara tisa pia akiwa nyuma ya staa wa Yanga, Heritier Makambo anayeongoza kwenye listi ya wafungaji akiwa nayo 11.

 

Kagere nyota wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya, ameliambia Championi Jumatano, kwamba kwake yeye binafsi hawazi kuchukua tuzo yoyote ile ndani ya klabu yake au ile ya mfungaji bora, badala yake anaelekeza mawazo yake katika kuipa Simba pointi tatu kwenye kila mechi yake.

 

“Sina mawazo ya kuwa mfungaji bora wala siwazi kwamba ninataka kuchukua tuzo ya aina yoyote nikiwa hapa.

 

“Kitu kikubwa ambacho ninafurahia ni kuona nakuwa sehemu ya msaada kwa Simba kwenye kupatikana kwa pointi tatu, tukishinda mechi yetu na mimi kufunga au kutoa pasi ya bao hapo ndipo ninajisikia vizuri na kusababisha hata nisiwaze juu ya kupata tuzo yoyote,” alisema Kagere.

Stori na Said Ally, Dar es Salaam

Comments are closed.