The House of Favourite Newspapers

Kagere, Ajibu Wabadili Mfumo Simba

BAADA ya kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar, Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, amesema sasa nguvu na akili zao wanaelekeza katika mchezo unaofuata dhidi ya Biashara United ya Mara na amepanga kubadili mfumo wa kikosi chake.

 

Simba ilikuwa haijapata ushindi dhidi ya Kagera katika msimu uliopita, kitu ambacho kiliwafanya kuhakikisha wanavunja mwiko katika uwanja huo wa Kaitaba huko Kagera.

Timu hiyo inatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Karume uliopo Musoma kuvaana na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara huku mshambuliaji tishio Meddie Kagere na kiungo Ibrahim Ajibu ambaye alianza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi hicho katika mchezo dhidi ya Kagera na kuonyesha uwezo mkubwa.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Aussems alisema amefurahishwa na viwango vya wachezaji wake walivyovionyesha ikiwemo kucheza kwa nidhamu kubwa iliyowawezesha kuvunja rekodi ya miaka miwili iliyopita kwenye uwanja huo.

 

Aussems alisema amepanga kuvuna pointi tatu katika michezo yote inayofuata watakayocheza ugenini baada ya kuwafunga Kagera kwa lengo la kukaa kileleni hadi mwishoni mwa msimu huu.

Aliongeza kuwa tayari ameachana na Kagera, hivi sasa nguvu zake za maandalizi ya kikosi chake amezielekeza kwenye mchezo wa Biashara, lengo ni kulitetea taji hilo la ubingwa.

 

“Nafahamu Biashara wamejiandaa na sisi pia tumejiandaa kwa lengo la kupata ushindi ambacho ndiyo kitu cha msingi, ninachokiangalia hivi sasa ili kuhakikisha tunachukua ubingwa wetu.

 

“Ninaendelea kukiboresha kikosi changu kwa lengo la kupata ushindi mwingine kwa kuwapa mbinu mbadala, tunakwenda kuwavaa Biashara wenye ‘pitch’ mbovu, hivyo ni lazima mfumo na aina ya uchezaji ubadilike,” alisema Aussems.

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Comments are closed.