The House of Favourite Newspapers

40 ya King Salah wa Zamaradi Yatikisa – Video

MASTAA wa Bongo Fleva na Bongo movies wamemiminika nyumbani kwa Mtangazaji, Zamaradi Mketema kwa ajili ya kuungana naye kusherehekea 40 ya mtoto wake, King Salah nyumbani kwake maeneo ya Bunju B, jijini Dar es Salaam.

King Salah ni mtoto wa tatu wa Zamaradi ambaye amezaa na mumewe aitwaye Shabani. Mtoto wake wa kwanza anaitwa Juju na wa pili anaitwa Shuby.

Baadhi ya mastaa hao ni Shamsa Ford, irene Paul, Kajala Masanja, Faiza Ally, Ester Kiama, Lamatha, Odama, Mama Rola, Halima Yahya ‘Davina’, Jimmy Mafufu, mwandishi wa Global Publishers na global TV Online, Immelda Mtema wa wengine kibao.

Comments are closed.