The House of Favourite Newspapers

Facebook Yafikisha Watumiaji Bilioni 1.8

zuckerberg-at-mobile-world-congress
Tajiri namba sita duniani, Mark Zuckerberg.
jumpfacebook1-jumbo
Wafanyakazi wa kampuni ya Facebook inc wakielekezana jambo.
20140227-facebook-paper-engineers-0110edit
Wafanyakazi wakiendelea na kazi.

25fb9 Ubao wa kuandika chochote.

Mitandao ya kijamii inayomilikiwa na tajiri namba sita duniani mwenye utajiri wa Dola za Marekani bilioni 52.2 ambazo ni sawa na Shilingi trilioni 114 za Tanzania, Mark Zuckerberg (32), inaonyesha kukua kwa kasi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Novemba 2 mwaka huu iliyotolewa kupitia ukurasa wa Facebook wa Mark Zuckerberg, inaonyesha mtandao wa Facebook umekua na kufikia watu bilioni 1.8, ambapo Whatsap imefikia bilioni 1, Facebook Messenger bilioni moja na Instagram milioni 500.

Watumiaji wa mitandao hiyo wamekuwa wakipendelea kuangalia vipande vya video na ku-‘share’ kila siku.
Malengo ya mitandao hiyo ni kuongeza idadi zaidi ya watu wanayoitumia na kila siku wanaendelea kuiboresha kila siku.

halotel-1

Comments are closed.